watanashati

watanashati

tengeneza website

tengeneza website

Tuesday, November 18, 2014

EXTRA BONGO YAJA KIVINGINE

 

 
Kama ulidhani ukimya wa Extra Bongo ni kifo cha bendi basi andika maumivu, bendi inakuja kivingine kabisa ambapo mwishoni mwa wiki hii inaingia kambini ikiwa na wasanii mchanganyiko wapya na wa zamani.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Chocky ameiambia Wataanashati wa Mujini kuwa bendi yake ilisitisha maonyesho baada ya kufiwa na mkewe (Mama Shuu) ambaye nae mkurugenzi wa bendi hiyo.
“Tunaingia kambini wiki ijayo (wiki hii), kambi ambayo haitazidi wiki mbili ikiwa ni maalum kwaajili ya wanamuziki kutambuana na kushikana pamoja na kutengeneza japo nyimbo chache mpya,” alisema Chocky na kuongeza kuwa wataanza rasmi maonyesho yao mwezi Disemba.
“Tuna wasanii wapya kutoka nje ya nchi na wachache wa hapa nyumbani, tumesajili kwa kuzingatia mahitaji ya bendi, hatujakurupuka. Lengo letu ni kuwa na kikosi kidogo lakini cha watu wachapakazi,” alifafanua Ally Chocky.
 
 

No comments:

Post a Comment