watanashati

watanashati

tengeneza website

tengeneza website

Wednesday, November 19, 2014

AMFUMANIA MUMEWE, ASAULA!

HATARI! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine
Mwanamke anayejulikana kwa jina la Tatu Ikoko akitishia kusaula mbele ya watu.
Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.
“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani,  akaanzisha vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.
Tatu Ikoko akiwa katika hali ya kuvurugwa baada ya kumfuma mumewe na hawara.
“Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake  walimshika na kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo na waliachana kwa tabia hiyo.
Majirani wakimsitiri Tatu Ikoko.
“Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,” kilisema chanzo hicho

SERIKALI KUDHIBITI UTOROSHAJI WA MADINI NJE YA NCHI


Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava(katikati)akikata utepe kufungua Maonesho ya Tatu ya Madini ya Vito ya kimataifa mkoani Arusha.
Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paul Massanja(kushoto)akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Vito jijini Arusha.
Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara kutoka nchini DRC.
Meneja Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini,Badra Masoud(kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa sekta ya madini nchini,Pandit katikati ni Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paulo Massanja.
Serikali imekua ikipoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee.  Kamishna wa Madini nchini,Eng Paul Massanja amesema leo wakati wa maonesho ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Amesema kwa takwimu za mwaka 2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni wakati nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India ilijikusanyia kitita cha dola 300 milioni. 
"Wote mnafahamu haya madini yanapatikana Tanzania pekee huu ni ushahidi kuwa kumekuwa na utoroshwaji wa madini haya kwa kiwango kikubwa jambo linalotunyima mapato ya kutosha"anasema Eng Massanja

Hata hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.

PICHA/HABARI: SHAKOOR JONGO

MISS TANZANIA 2013 JETS INTO LONDON TO FOR THE MISS WORLD PAGEANT

Miss Tanzania Happiness Watimanywa signs the guests book at the Tanzania High Commission in London as the High Commissioner H.E Ambassador Peter Kallaghe looks on.
The Tanzania High Commissioner to the UK H.E Ambassador Peter Kallaghe hands over the national flag to Miss Tanzania Happiness Watimanywa
Today Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa  paid a courtesy call to the Tanzania High Commission in London where  She was welcomed  by the High Commissioner H.E Ambassador Peter Kallaghe.
During their meeting Miss Happiness was able to update the  High Commissioner about her mission to represent Tanzania as a country at the coveted  64th edition of Miss world beauty pageant that will take place in early December.
She had won the national pageant last year and as the new system goes, she  represents the country this year, as would Miss Tanzania 2014 do the same next year.
In return the High Commissioner pledged to  her the all  the support and backing of the Tanzania mission in London and wished her all the best. Thereafter a national flag was presented to her.
anzania may not win the Miss World crown this year or ever or even surpass this year’s record in many years to come but we must learn to celebrate what we have achieved now as we prepare and plan for the future. Tanzanians must not wait for Tanzania to win the Miss World before celebrating, let’s celebrate now and leave the future to take care of itself.Lets all support Happiness Watimanywa

HAKUNA NCHI INAYOWEZA KUSIMAMA PEKE YAKE-BAN KI MOON


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, wajumbe wa kamati hiyo akiwamo Mhe, Spika Anne Makinda ( Mb) walikutana kwa siku mbili  hapa Umoja wa Mataifa
Pamoja na  kuzungumza na Katibu Mkuu,maspika wanaounda kamati ya maandalizi walipata fursa
pia
ya kubadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan  Eliasson
Spika wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ( Mb) akisalimia na Katibu Mkuu, Ban Ki Moon
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Bw. Jan Eliasson akisalimiana na  Mhe. Anne Makinda ( Mb) Spika wa Bunge  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Spika  Anne Makinda ( Mb) akibadilishana mawazo na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dr. Theo-Ben Gurirab
Pamoja jukumu kubwa la  mkutano wa  kamati ya maandalizi, Mhe. Spika alipata nafasi ya  kufika  katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo alipokelewa na Naibu  Mwakilishi wa Kudumu  Balozi, RamadhaniMwinyi. Hapa Mhe. Spika  akisaini kitabu cha wageni na pembeni yake ni Balozi Ramadhan Mwinyi na  aliyeketi ni Bw. Eliufoo Ukhotya kutoka Ofisi ya Spika.

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA WATANASHATI WA MUJINI

 Mwenyekiti wa Watanashati wa Mujini Adel Alex alipotembelea mkoani Mbeya

 Picha mbili tofauti zikimuonyesha memba wa Watanashati wa Mujini anayejulikana kwa jina la Noordin akifurahia sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

MBUNGE WA KIBAHA AWAPA KIWANJA WATANASHATI WA MJINI

Wasanii wa filamu Dokta Cheni na Chiki Mchoma, wakila sahani moja ya futari na watoto yatima.

Mshereheshaji maarufu Bongo, Zipompapompa, akipata futari na Watanashati wa Mujini wenzake
Mbunge wa Kibaha Mheshimiwa Slyvester Koka, akiongea jambo wakati akiwapatia zawadi ya kiwanja wasanii wanaounda Group la Watanashati wa mjini kupitia mtandao wa kijamii wa Whats app unaopatikana katika simu za mikononi za Smart Phone.
Dokta Cheni akikabidhi keki kwa mmoja wa watoto yatima waliohudhuria kwenye futari hiyo katika ukumbi wa Trip S Kibaha.
Msanii wa filamu Bongo, Michael Sangu akijitambulisha kwa watoto yatima.
Baadhi ya watoto yatima wakipata futari.
Mmoja wa wanachama  wanaounda kundi hilo akigawa futari.
 Mtangazaji wa TBC 1, Chacha Maginga ambaye alikuwa katibu wa kundi hili kabla hajajihudhuru akiongea jambo kwa niaba ya Watanashati wa Mjini.
Mlezi wa Group hilo Mama Cynthia Henjewele (kushoto), akila futari na mke wa Mbunge Belina Koka kwenye hafla hiyo.

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mheshimiwa Slyvester Koka, usiku wa kuamkia leo alitoa shavu kwa wanachama  wanaounda kundi la Watanashati wa Mjini kwa kuwapatia Ofa ya kiwanja watakachojengea jengo la kulelea watoto yatima Kibaha mjini.
Wanachama  wanaounda kundi hilo ni Adel Alex, Michael Sangu, Said Mdoe, Lizzy Baby, Berna Piere, Jodete Dominic, Mc Zipompapompa, Dotnata Posh, Nelly, Enock Bwigane, Noordin, Munirah, Dudith Fraancis, Montana, na wengine tu.
Akizungumza kwa niaba ya Watanashati, aliyekuwa katibu wa kundi hilo Chacha alisema kuwa kundi lina zaidi ya watu 70, na nia kubwa yao ni nikuhakikisha wanasaidiana  na

pia kuwekeza katika kutatua matitizo madogo madogo ya watoto yatima.





PICHA/HABARI: SHAKOOR JONGO

Tuesday, November 18, 2014

EXTRA BONGO YAJA KIVINGINE

 

 
Kama ulidhani ukimya wa Extra Bongo ni kifo cha bendi basi andika maumivu, bendi inakuja kivingine kabisa ambapo mwishoni mwa wiki hii inaingia kambini ikiwa na wasanii mchanganyiko wapya na wa zamani.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Chocky ameiambia Wataanashati wa Mujini kuwa bendi yake ilisitisha maonyesho baada ya kufiwa na mkewe (Mama Shuu) ambaye nae mkurugenzi wa bendi hiyo.
“Tunaingia kambini wiki ijayo (wiki hii), kambi ambayo haitazidi wiki mbili ikiwa ni maalum kwaajili ya wanamuziki kutambuana na kushikana pamoja na kutengeneza japo nyimbo chache mpya,” alisema Chocky na kuongeza kuwa wataanza rasmi maonyesho yao mwezi Disemba.
“Tuna wasanii wapya kutoka nje ya nchi na wachache wa hapa nyumbani, tumesajili kwa kuzingatia mahitaji ya bendi, hatujakurupuka. Lengo letu ni kuwa na kikosi kidogo lakini cha watu wachapakazi,” alifafanua Ally Chocky.