Wasanii wa filamu Dokta Cheni na Chiki Mchoma, wakila sahani moja ya futari na watoto yatima.
Mshereheshaji maarufu Bongo, Zipompapompa, akipata futari na Watanashati wa Mujini wenzake
Mbunge
wa Kibaha Mheshimiwa Slyvester Koka, akiongea jambo wakati akiwapatia
zawadi ya kiwanja wasanii wanaounda Group la Watanashati wa mjini kupitia mtandao wa kijamii wa Whats app unaopatikana katika simu za mikononi za Smart Phone.
Dokta Cheni akikabidhi keki kwa mmoja wa watoto yatima waliohudhuria kwenye futari hiyo katika ukumbi wa Trip S Kibaha.
Msanii wa filamu Bongo, Michael Sangu akijitambulisha kwa watoto yatima.
Baadhi ya watoto yatima wakipata futari.
Mmoja wa wanachama wanaounda kundi hilo akigawa futari.
Mtangazaji wa TBC 1, Chacha Maginga ambaye alikuwa katibu wa kundi hili kabla hajajihudhuru akiongea jambo kwa niaba ya Watanashati wa Mjini.
Mlezi wa Group hilo Mama Cynthia Henjewele (kushoto), akila futari na mke wa Mbunge Belina Koka kwenye hafla hiyo.
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mheshimiwa
Slyvester Koka, usiku wa kuamkia leo alitoa shavu kwa wanachama wanaounda
kundi la Watanashati wa Mjini kwa kuwapatia Ofa ya kiwanja
watakachojengea jengo la kulelea watoto yatima Kibaha mjini.
Wanachama wanaounda kundi hilo ni Adel Alex, Michael Sangu, Said Mdoe, Lizzy Baby, Berna Piere, Jodete Dominic, Mc Zipompapompa, Dotnata Posh, Nelly, Enock Bwigane, Noordin, Munirah, Dudith Fraancis, Montana, na wengine tu.
Akizungumza kwa niaba ya Watanashati, aliyekuwa katibu wa kundi hilo
Chacha alisema kuwa kundi lina zaidi ya watu 70, na nia kubwa yao
ni nikuhakikisha wanasaidiana na
pia kuwekeza katika kutatua matitizo madogo madogo ya watoto yatima.
PICHA/HABARI: SHAKOOR JONGO
No comments:
Post a Comment