Serikali
imekua ikipoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini aina ya
Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee. Kamishna
wa Madini nchini,Eng Paul Massanja amesema leo wakati wa maonesho ya
madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na
washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
Amesema kwa
takwimu za mwaka 2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni
wakati nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India
ilijikusanyia kitita cha dola 300 milioni.
"Wote
mnafahamu haya madini yanapatikana Tanzania pekee huu ni ushahidi kuwa
kumekuwa na utoroshwaji wa madini haya kwa kiwango kikubwa jambo
linalotunyima mapato ya kutosha"anasema Eng Massanja
Hata hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.

PICHA/HABARI: SHAKOOR JONGO
No comments:
Post a Comment