watanashati

watanashati

tengeneza website

tengeneza website

Sunday, November 9, 2014

HII NDIO BARABARA ILIYOKARABATIWA KWA MILIONI 90 UKONGA MAZIZINI- MOSHI BAR

 
Hii ndio ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo
tu ya hizo kilometa tatu. 

Meya Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao.
 
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changarawe awamu ya kwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinu ulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu. 
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar. 
Mwonekano wa Bara barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment